29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

REDKNAPP ALIKATAA BAO LA GIROUD

LONDON, ENGLAND


 

giroudNYOTA wa zamani ambaye aliwika katika klabu ya Liverpool na Tottenham, Jamie Redknapp, amedai bao la mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud, bado halijafikia kuingia katika mabao 20 bora yaliyowahi kufungwa kwenye soka.

Giroud amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kufunga bao mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Crystal Palace, huku Arsenal ikishinda mabao 2-0.

Bao hilo ambalo lilipewa jina la ‘scorpion kick’, halina tofauti kubwa na lile ambalo lilifungwa na kiungo wa Man United, Henrikh Mkhitaryan, Desemba 26, mwaka jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland, tofauti ya bao hilo ni kwamba, Giroud la kwake lilianza kugonga mwamba huku Mkhitaryan likiingia moja kwa moja wavuni.

Lakini kwa upande wa Redknapp, amedai kuwa bao la Giroud ni bora ila haliwezi kuingia katika orodha ya mabao 20 bora duniani ambayo yaliwahi kufungwa.

“Bao la Giroud la ‘scorpion kick’ dhidi ya Crystal Palace ni bao bora ambalo sijaliona kwa hivi karibuni. Hakuna hata mmoja ambaye alidhani kama mchezaji huyo angeweza kufanya vile.

“Sina tatizo lolote na Giroud, lakini ukweli ni kwamba bao hilo halinifanyi niliweke kwenye orodha ya mabao 20 bora katika michuano ya ligi kuu. Ukweli ni kwamba, Giroud alikuwa na bahati kwa kuwa hakudhani kama mpira atapigiwa kwa nyuma.

“Hata kama ni bao bora lakini siwezi kulilinganisha na lile ambalo aliwahi kulifunga Thierry Henry katika mchezo dhidi ya Manchester United au bao ambalo alilifunga Wayne Rooney dhidi ya Manchester City pamoja na lile ambalo alilifunga Dele Alli mwaka jana dhidi ya Crystal Palacem pamoja na orodha kubwa ambayo ninaweza kuitaja,” alisema Redknapp.

Hata hivyo, kwa upande wa Giroud mwenyewe alidai kuwa anaamini ilikuwa ni bahati kuweza kufunga bao la aina hiyo, ila anashukuru kuwa ameisaidia timu yake kujipatia alama tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles