24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Makonda awa mbogo

MAKONDANA GRACE SHITUNDU, DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefuta kibali cha shughuli za ujenzi cha Kampuni ya Ukandarasi ya Inshinomya Co. Ltd baada ya kubainika kujenga barabara chini ya kiwango.

Kwa uamuzi huo, kampuni hiyo sasa haiwezi tena kufanya kazi za ujenzi wa barabara katika halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam.

Sambamba na hatua hiyo, Makonda amesitisha zabuni ya ujezi wa barabara kwa kampuni nyingine tatu za Germinex Construction Ltd, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction hadi atakapoamua vinginevyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema barabara nyingi zilizojengwa na kampuni hizo zimejengwa chini ya kiwango na zitaharibika haraka.

“Makampuni haya yamekuwa yakifanya ujenzi wa barabara chini ya kiwango ili ziharibike mapema na wao waweze kupata zabuni nyingine.

“Hatuwezi kufika popote katika maendeleo kwa kuwa na barabara zenye viwango vya chini halafu tukaendelea kuziangalia hizo kampuni ambazo wakati zinaendelea na ujenzi tayari zinakuwa zimeanza kuharibika,” alisema Makonda.

Alisema barabara za Mkoa wa  Dar es Salaam nyingi zina mashimo kwa sababu kampuni zinazopewa tenda zinafanya kazi kwa mazoea.

Kwa upande wa barabara ambazo tayari zimeharibika, Makonda aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kuzikarabati katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

“Pamoja na kuzisimamisha kampuni hizi nawataka wakurugenzi wote kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja katika Mkoa wa Dar es Salaam hakuna barabara iliyokuwa na mashimo,” alisema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles