31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jipu jipya la watumishi hewa

mongellaNA JUDITH NYANGE, MWANZA

MKOA wa Mwanza umebaini uwepo wa watumishi hewa wapya 1,057 baada ya kurejea kwa zoezi la uhakiki.

Watumishi hao hewa wamelipwa jumla ya Sh bilioni 2.2 katika kipindi chote walichoingizwa kwenye malipo ya mishahara ya watumishi wa umma bila kuwepo katika vituo vyao vya kazi.

Idadi hiyo ni mara tatu zaidi ya ile ya awali ya ripoti za wakuu wa mikoa zilizowasilishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Ripoti hiyo ya awali iliwasilishwa Aprili mosi, 2016, jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuhakiki watumishi hewa nchi nzima ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliwasilisha orodha ya watumishi 334.

Akitoa salamu za Mkoa wa Mwanza jana kwa watumishi katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyikia ofisini kwake, Mongella alisema ongezeko la idadi ya watumishi hewa limetokana na taarifa  ya watumishi waliolipwa Februari, mwaka 2016.

Alisema taarifa iliyotolewa kwenye Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri ilionyesha kuwepo watumishi 28,068 kwa mkoa mzima huku upande wa halmashauri wakiwa 27,416  na mkoa ukiwa na watumishi 652.

Mongella alisema watumishi waliofika kuhakikiwa walikuwa 26,359 na 1,057  hawakufika.

“Watumishi 367 kati ya 1,057 ambao hawakufika kuhakikiwa walilipwa Sh bilioni 2.2 bila kuwepo katika vituo vyao vya kazi, watoro 214 walilipwa Sh bilioni 1.6, wastaafu 74 Sh milioni 226.7, walioacha kazi 10 walilipwa Sh milioni 54.4, waliofariki 33 Sh milioni 64.5, waliogombea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wawili na walilipwa Sh milioni 12.1, wasiojulikana kwa mwajiri 31, walilipwa Sh milioni 207 na waliofukuzwa kazi watatu ambao wawili taarifa zao hazikupatikana na mmoja alilipwa Sh 332,100.

“Wapo watumishi 689 ambao hawakufika kwenye uhakiki kutokana na sababu mbalimbali ambapo 416 walihama, 29 wako masomoni, 18 wagonjwa, 221 wasiokuwa na sababu na watano waliokuwa likizo lakini walistahili kulipwa.

“Watumishi 35 hawakuhakikiwa katika sekretarieti ya mkoa kati yao watumishi walioazimwa ni wawili, 20 wako masomoni, wanane wamehama vituo vya kazi, mgonjwa mmoja, mstaafu mmoja, waliofariki mmoja ambaye akaunti yake iliingizwa Sh milioni 3.9 na aliyeachishwa kazi mmoja ambaye pia aliingiziwa Sh milioni 3.5,” alisema Mongella.

Aliyataja mambo mengine yaliyobainishwa na tume wakati wa uhakiki ni pamoja na uwepo wa  watumishi waliokopa mikopo benki ambao hawapo katika utumishi wa umma, waliolipwa mapunjo ya mishahara yao mara mbili na watumishi ambao hawakufika kuhakikiwa bila sababu yoyote.

“Wapo watumishi 13 katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Kwimba ambao wamekopa mikopo benki wakati hawapo katika utumishi wa umma, watumishi 72 walilipwa mapunjo ya mishahara katika Halmashauri ya Magu kupitia akaunti zao za benki na vile vile wakalipwa dirishani (dauble payment) pamoja na  watumishi 221 waliogoma kufika eneo la uhakiki bila sababu zotote,” alisema Mongella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles