27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa wa Serikali kizimbani kwa udanganyifu

NA MURUWA THOMAS, NZEGA

OFISA Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Alloys Andew Kwezi, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisomewa mashtaka na wakili wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edson Mapalala, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Saraphina Nsana, mtuhumiwa alidaiwa kutenda kosa hilo Septemba 24, mwaka 2014 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati akiwa mtumishi mwenye cheo cha Ofisa Utumishi.

Wakili Mapalala alidai kuwa awali mtuhumiwa alikuwa ofisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ambako alijipatia fedha Sh 3,025,000 kwa njia ya udanganyifu.

Mtuhumiwa alikana shtaka hilo kwa kuieleza mahakama kuwa alichukua fedha kama stahiki yake ya malipo kwa ajili ya kwenda likizo.

Shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa Juni 29, mwaka huu na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana ya Sh milioni 4 mdhamini mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles