30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanajeshi kortini kwa ubakaji

MANENO SELANYIKA NA BARAKA MASSAWE (TSJ), DAR

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) wa kambi ya Lugalo, Hamis Omary (31), amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumbaka mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka minne.

Mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, wakili wa Serikali, Amani Mghamba, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei, 31 mwaka huu eneo la Kawe, Wilaya ya Kinondoni.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili Mghamba alidai kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kilichomsababishia maumivu makali mtoto huyo.

Mtuhumiwa alikana shtaka linalomkabili na Hakimu Kiliwa alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo lina dhamana hivyo alimtaka mtuhumiwa awe na wadhamini wawili wanaotoka serikalini au katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.

“Kila mdhamini anatakiwa aje na barua kutoka kwa mwajiri wake kisha wataweka ahadi ya maandishi ya Sh milioni 2 kwa kila mmoja,” alisema Hakimu Kiliwa.

Mtuhumiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na alirejeshwa mahabusu hadi Julai 8 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles