26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rayvan aishukuru Basata kuruhusu WCB kufanya matamasha nje ya nchi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny amelishukuru Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kuruhusu yeye na wasanii wenzake kutoka lebo hiyo kufanya Tamasha la Wasafi Festival katika miji ya Mombasa, Nairobi na nchini Comoro ambapo awali walizuiliwa.

Desemba 18 mwaka 2018, Basata walitoa barua ya kuwazuia Rayvanny na kiongozi wa lebo hiyo, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz kutofanya tamasha lolote ndani na nje ya nchi baada ya kutumbuiza wimbo wa Mwanza walioshirikiana Rayvan na Diamond kutokana na ukosefu wa maadili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo, Jumatatu Desemba 7, Rayvann ametuma ujumbe kulishukuru baraza hilo kwa kuwapatia ruhusa ya kufanya tamasha hilo nje ya nchi ambayo awali walitakiwa kutokulifanya kutokana na makosa waliyotenda.

“Tulitakiwa tusifanye tamasha hilo lakini Basata kwa upendo wenu mlituruhusu kufanya, nitoe shukrani zangu za dhati kwenu maana bila nyie kutupa ruhusa ni mengi yangetukuta vijana wenu.

“Lakini pamoja na yote yaliyotokea kwetu ni kama darasa la kujua wapi tulipoteleza ili mbeleni lisijirudie kosa kama tulilofanya, tuna ahidi kuwa vijana bora na mfano kwa jamii hususani katika maadili, tuaamini mnatupenda vijana wenu na mnatamani tufike mbali katika sanaa,” ameandika Rayvanny.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amethibitisha Baraza hilo kutoa kibali kwa wasanii hao kufanya matamasha nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles