27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wastaafu waandamana hadi NSSF kushinikiza walipwe mafao yao

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Zaidi ya wanachama 200 wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekusanyika katika Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni wakishinikiza kulipwa mafao yao.

Wastaafu hao wamekusanyika leo kuanzia saa sita mchana katika ofisi hizo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ambapo wako waliostaafu kuanzia mwaka jana kurudi nyuma ambapo pamoja na mambo mengune wamedai hawajui ni kwanini hawalipwi mafao yao wakati Rais John Magufuli ametangaza wapewe mafao yao kwa wakati.

Akizungumza na Mtanzania Digital mmoja wa wastaafu hao, Khamis Khamis, amesema yeye amestaafu tangu Juni mwaka 2018 lakini kila anapoenda kudai mafao yake anapigwa tarehe hali inayomfanya anashindwa kulipia watoto ada za shule ama kufungua biashara.

Amesema wamekusanyika ili kupatiwa stahiki zao huku wakishinikiza kitumike kikotoo cha zamani na sio kile cha asilimia 33.3 kwani mtu anakuwa anadai fedha nyingi ila anapewa kidogo sababu tu sheria hairuhusu wakati Rais Magufuli alisema kila anayestaafu anapaswa kulipwa mafao yake kwa wakati

“Wafuate kile Rais Magufuli alichosema kuwa mtu anapostaafu apewe stahiki zake asilimia 100 ili kila mtu akajikimu na maisha yake na tunaomba uongozi wa NSSF watoe tamko kutujuza sisi mafao yetu tunapewa lini kwasababu tumechoka kuzungushwa kila siku,” amesema Khamis.

Kwa upande wake Ashura Nzuruni amesema wanadai haki zao na kuhusu asilimia 33 hawaielewi na inakuwaje wanaenda kinyume na Rais alivyosema ilihali aliagiza wastaafu wapewe haki zao.

“Sisi tunataka haki zetu zote hawawezi kutuambia watarithi watoto wetu, tukifa je, tunataka sisi tuliofanya kazi wenyewe tupewe nguvu zetu, mtu anadai Sh milioni tatu anapewa 90,000 sababu wametumia sheria ya asilimia 33 ambayo hatuielewi kwa kweli,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni, Hiza Kiluwasha, alipofuatwa alikataa kuzungumzia suala hilo huku akidai yuko ‘bize’ kuwahudumia wateja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles