29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara watakiwa kupenda wanachokifanya kuongeza ubora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAFANYABIASHARA na wajasiriamali nchini wametakiwa kupenda kile wanachokifanya ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora, wanakuza mitaji pamoja na kupambana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2024 na Mkufunzi wa mambo ya Tehama na Teknolojia, Mihayo Wilmore wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Shirika linalojihusisha na Utoaji wa Mafunzo na Ujunzi kwa Wajasiriamali la CEED Tanzania.

Wilmore alisema bila mfanyabiashara kupenda kile anachokifanya inakuwa ni ngumu kuendeleza biashara yake na kukuza mitaji hivyo ujikuta anakwama na kupoteza hata wateja aliyowapata.

“Kama mtu upendi kile kitu unachokifanya ni vigumu sana kufanikiwa kwa sababu unakuta wakati fulani unakumbana na changamoto nyingi hata kukata tamaa kabisa sasa kama upendi hicho unachofanya lazima inakiuwa ngumu kusonga mbdele, ni muhimu kuhakikisha unachokifanya unakipenda na kukiheshimu,” alisema Wilmore.

Aidha Wilmore aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia mitandao ya kijamii kutafuta fursa, kujenga mahusiano mazuri na wateja wao pamoja na kutangaza biashara kwa ujumla ili kujikwamua kiuchumi.

“Tuna mitandao mingi ya kijamii kama Tiktok, Instagram, Linkedln na mingine mingi, ni miuhimu wafanyabiashara wakatambua ni mtandao upi unatumika kwa ajili ya biashara, mtandao mzuri kwa ajili ya biashara ni Linkedln ila watanzania wengi hawajui na hawapo humo.

“Mtandao wa kijamii mwingine ambao ni mzuri kwa biashara ni Instagram, lakini nawaomba wajasiriamali wasichanganye biashara na mambo yao binafsi katika kurasa zao za kijamii,” alisema Wilmore

Naye Mkurugenzi wa Shirika la CEED Tanzania, Atiba Amalile alisema  kupitia mradi wa miaka mitano wa Daraja Impact unaolenga kusaidia biashara ndogo na za Kati Tanzania (SMEs) wamefanikiwa kuwakutanisha wajasiriamali na wafanyabishara kwa lengo la kuwapatia elimu hasa ya masuala ya tekonolojia na tehama.

Amalile alisema mradi huo wa Daraja Impact unalenga kutoa mitaji na usaidizi wa kiufundi ili kuendeleza ushirikishwaji wa kiuchumi na uwezeshaji kwa biashara zenye tija kwa wanawake na vijana hapa nchini.

“Mradi huu wa Daraja Impact unafadhiliwa na Swiss Confederation linalowakilishwa na Idara ya Mambo ya Nje ya  Uswisi (SDC) kupitia Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania, unatekelezwa na Small Enterprise Assistance Fund (SEAF) kwa ushirikiano na Shirika la AlphaMundi  (AMF),” alisema Amalile

Kwa upande wake Fortunata Mmari ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, alisema kupitia elimu aliyoipata imemsaidia kupata uelewa hasa wa namna bora wa kuboresha utengenezaji unga wa nafaka na uuzaji wa nafaka kwa ujumla.kwa kutumia mifumo na mbinu mbalimbali za ubunifu na teknolojia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles