Ray aigeukia familia yake

0
909

Na GLORY MLAY

MSANII wa filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema anacho kiangalia kwa sasa ni namna ya kuitunza familia yake na sio kuangaika na umaarufu.

Msanii huyo ambaye alikuwa anakimbizana na marehemu Kanumba katika kazi zao za filamu amesema tayari amepata umaarufu wa kutosha, hivyo sasa anataka kuipigania familia yake.

“Sina mpango na umaarufu tena, tayari kipindi cha nyuma nilisifika sana kupitia kazi yangu ya filamu ila kwa sasa naangalia ni jinsi gani nitaitunza familia.

“Lazima niwe baba ninayejitambua, hivyo umaarufu na waachia wasanii chipukizi kwa sasa ambao hawana majina makubwa,” alisema msanii huyo.

Aliongeza kwa kusema muda huu anaweka pembeni masuala ya filamu, lakini anaweza kurudi akiweka vizuri mambo yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here