27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Lampard afurahishwa na chipukizi Chelsea

DUBLIN, IRELAND

KOCHA mpya wa timu ya Chelsea, Frank Lampard, amedai kuvutiwa na kiwango walicho kionesha wachezaji wake chipukizi kwenye mchezo wa kwanza wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi dhidi ya Bohemians.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa juzi huko mjini Dublin nchini Ireland, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, lakini kocha huyo amedai wachezaji wake chipukizi ambao anaamini atawatumia kwenye msimu mpya wa ligi walionesha kiwango kizuri.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Michy Batshuayi dakika ya nane, lakini wapinzani hao walifanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 89 kupitia kwa staa wao Eric Molloy.

“Ni moja ya mchezo bora wa maandalizi ya msimu, tumepata mapokezi mazuri na mashabiki walitoa sapoti ya kutosha tunawashukuru sana. Kwa upande mwingine naweza kusema ulikuwa mchezo mgumu kwetu japokuwa tulikuwa wa kwanza kupata bao, lakini wapinzani walionesha wapambanaji.

“Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi yetu ya msimu mpya wa ligi, nimevutiwa sana na kiwango walichokionesha vijana wangu, sikukitarajia.

“Kikubwa wachezaji bado hawapo fiti kwa kuwa wengi wao walikuwa kwenye mapumziko ya muda mrefu, lakini ninaamini siku za hivi karibuni watarudi katika hali ya mchezo na kuja kuwa fiti, hivi ndivyo maandalizi ya msimu yalivyo.

“Tulitaka kushinda mchezo huo, lakini haikuwa lazima sana kwa kuwa kitu muhimu ni kuhakikisha miili ya wachezaji inakuwa sawa baada ya kutoka mapumzikoni ili waje kuwa bora wakati wa ligi na michuano mingine,” alisema Lampard.

Wachezaji wa Chelsea ambao wapo kwenye ziara hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ni 35, lakini katika mchezo huo wa juzi walipata nafasi ya kucheza wachezaji 22, hivyo Lampard amedai wengine watakuja kupata nafasi kwenye michezo mingine ikiwa pamoja na ule wa Jumamosi wiki hii dhidi ya St Patrick.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles