28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia mgeni rasmi tamasha la michezo la wanawake

Na Jescar Victor,  TUDARCo

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua tamasha la kwanza la michezo la wanawake linaloitwa  Tanzanite litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Septemba 16 hadi 18, 2021 huku uzinduzi rasmi ukifanyika Jumamosi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk.Hassan Abbasi, ameyasema hayo leo Septemba 15, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Toka aingie madarakani Rais Samia ameonesha nia ya dhati ya kuinua michezo kwa wanawake hivyo amekubali kuja kuzindua tamasha hili ambalo litaanza tarehe 16-18 Septemba, 2021,” amefafanua Dk. Abbasi.

Amesema tamasha hilo la kihistoria limesheheni michezo mbalimbali ikiwemo riadha, ndondi, soka, netiboli, mpira wa kikapu, wavu, karate, makomando wa kike, kuvuta kamba, rede na mingine mingi.

“Katika kunogesha tamasha hilo watakuwepo wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya huku asilimia zaidi ya 98 wakiwa ni wakike ambao nao wataonesha uwezo wao na orodha kamili itatewa baadaye,” amesema Dk. Abbasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles