23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Nitagombea Urais 2025, Wameanza kutuchokoza

Judith Siaga na Juliana Samwely,TUDARCo

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Samia ametangaza kuwania nafasi hiyo leo Jumatano Septemba 15, 2021 kwenye Kongamano la Siku ya Demokrasi duniania ambalo kitaifa limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, likienda sambamba na kukabidhiwa tuzo kwa rais.

Kauli ya Rais Samia imekuja baada ya mwezi uliopita Gazete la Chama Cha Mapinduzi(CCM) la Uhuru la Agosti 11 kuandika kuwa kiongozi huyo hana mpango wa kugombea urais 2025.

Katika ukurasa wake wa mbele wa gazeti hilo toleo la Agosti 11, lilichapisha habari yenye kichwa kilichosomeka kuwa “Sina wazo la kiwania urais 2025”- Samia. Hatua ambayo ilipelekea gazeti hilo kwanza kusimamishwa kwa wiki moja na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo hatua iliyoenda sambamba na kusimamishwa kwa watendaji wake, kisha baadaye Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Gerson Msigwa alistisha leseni ya gazeti hilo kwa muda wa siku 14.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Rais Samia amesema rais mwanamke atawekwa mwaka 2025 na kwamba wakifanya vitu vyao vizuri ikiwamo kushikamana kumuweka rais wetu watakutana hapo kwa furaha kubwa.

“Leo hapa mmempa rais tuzo, rais mwamnamke kwa furaha na bashasha na furaha kubwa, lakini nataka niwaambie wanawake bado hatujaweka rais mwanamke. Rias Mwanamke huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na matakwa ya katiba.

“…wanawake oyeee…tulichokichangia sisi na dada zetu na mama zetu kina mama Anna Abdallah ni ile kusukumaa… mpaka mwanamke akawa Makamu wa Rais(Samia Suluhu) ule ndio mchango mkubwa tumeufanya sisi wanawake. Lakini kufika hapa isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana tungefikia hapo kila mwaka tunakwenda ni hapo ni hapo…, sasa ndugu zangu rais mwanamke tutamuweka mwaka 2025,” amesema Rais Samia na kuongeza kuwa:

“…wanawake oyee…Tanzania oyeee, ndugu zangu mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti samia hatasimama nani kawaambia? Fadhila za Mungu zikija mkoni kwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu ndugu zangu, wanawake wamefanyakazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hizi, wanawake tumefanyakazi kubwa kujenga siasa za nchi hizi, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hizi, leo Mungu ametupa baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani,” amesema Samia.

Wakati huo huo Rais Samia amekabidhiwa tuzo kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini iliyotolewa Mwenyekiyi wa Azaki ya Tanzania Women Cross-Party Platform/ULINGO,Anna Abdallah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles