28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kusuka upya Serikali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

RAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema atafanya mabadiliko kwa baadhi ya viongozi wa Serikali yake ili kupata wale wanaoenda sambamba na kasi yake.

Dk. Samia ametoa angalizo hilo leo Desemba 8, 2022 katika Mkutano wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) uliohitimishwa leo jijini Dodoma ambapo amesema kuwa wanasafari ya miaka mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025, ili wananchi wawe mashuhuda wa yanayofanywa.

“Kubwa zaidi tunapokwenda kwa wananchi, ni wananchi wenyewe wanayosema serikali waliyofanya kwao, tofauti na utamaduni tuliokuwa nao nyuma, kwamba tunapokwenda kwa wananchi serikali ndio tunawaambiwa tumewafanyia, wakati mwingine wanashangaa hiki kimefanyika wapi,”amesema Dk. Samia.

Ameongeza kuwa mabadiliko hayo yatatoa nafasi kwa wananchi kuona na kutoa tathmini ya yaliyofanyika na wenyewe kuwa mashuhuda wa kila kinachofanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles