23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo-Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwajibika katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na maeneo yaliayoainishwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Desemba 8, 2022 katika Mkutano wa 10 wa chama hicho, uliofanyika jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya Serikali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika miradi ya maendeleo.

Amesema serikali itaendelea kushughulikia changamoto na kwamba serikali itaendelea kupokea maelekezo ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya serikali, utendaji wenye uadilifu na uaminifu.

Waziri Mkuu amemhakikisha Rais Samia kuwa wao kama watendaji wa serikali wataendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na kupokea maelezo, uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti tumeona kazi zako na tunaaendela kuamini kazi hizi zitaboreshwa uendelee kufanya kazi kwa amani na utulivu, wasaidizi wako tupo,” amesema Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles