Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema ataendeleza nia na azma yake ya utamaduni wa kusimaimia majadiliano ya kiungwana baina ya vyama vya siasa nchini.
Dk. Samia ambaye pia amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(CCM) amebainisha hayo leo Desemba 8, 2022 jijini Dodoma ambapo amesema lengola kufanya hivyo ni kutaka kuimarisha misingi ya demokrasia, umoja na maridhoano ya kitaifa nchini na kuondoa mawazo potofu kuwa demokrasia ni tume ya uchaguzi na uchaguzi pekee.
“Demokrasia ni utamaduni sio wa taasisi wala sio utaratibu za uchaguzi bali jinsi ya kuendesha mambo yetu nchini kwetu kwa mazingira yetu na rasilimali tulizo nazo, kushirikishana kuendesha mambo yetu, serikali na vyama wana wajibu wa kukuza utamaduni wa kuheshimiana, kuvumiliana, kuendeleza yenye maslahi kwa wananchi,”amesema Dk. Rais Samia.
Pia akatika hatua nyingine amevikumbushia kuwa utaratibu wa majadiliano haiivui CCM dhamana waliyopewa ya kuwa chama tawala, bali unawafanya kuvuta wengine (upinzani), wakae na kukubaliana namna ya kuendesha siasa kwa ustaarabu.