Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua jukwaa la kodi na uwekezaji mwaka huu, lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo kusaidia kuandaa bajeti ya mwaka 2024/2025.
Akizungumza jijini Arusha Februari 23, 2024 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya amesema jukwaa hilo ni utaratibu wa kawaida ambao unawahusisha wananchi na wadau wengi kutoa maoni yao.
Amesema jukwaa hilo litafanyika jijjni Dar es salaam na kushirikisha wadau 1000, wakiwemo wafanyabiashara,mabalozi, wadau sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi.
“Mpaka sasa tumeshapita katika kanda mbalimbali nchini, kwa ajili ya kukusanya maoni ya wadau na wananchi na Februari 27 na 28 itakua ni hitimisho,” amesema.