27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli amlilia Sitta

sitta-na-maguNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na kifo cha Spika mstaafu, Samuel Sitta.

Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Technical University of Munich, nchini Ujerumani, alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sitta na kwamba taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.

“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.

Pamoja ana Spika, Dk. Magufuli ametuma salamu za pole kwa mke wa marehemu, Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo na familia nzima ya marehemu, wabunge, wananchi wa Urambo na Watanzania kwa ujumla.

“Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na nawaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles