30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rafael Nadal atinga nusu fainali US Open

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA namba mbili kwa ubora wa mchezo wa tenisi duniani upande wa wanaume, Rafael Nadal, amefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya US baada ya kumshinda mpinzani wake Diego Schwartzman.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu ambayo ulitumia zaidi ya saa 2:30 na kumfanya Nadal ashinde kwa seti 6-4, 7-5, 6-2, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Arthur Ashe.

Mashindano hayo msimu huu yamekuwa na ushindani wa hali ya juu huku magwiji kama vile Roger Federer na Novak Djokovic wakitupwa nje, lakini Nadal ameweza kusonga mbele hatua inayofuata.

Nadal mwenye umri wa miaka 33, lengo lake kubwa ni kuhakikisha anatwaa taji hilo kubwa la Grand Slam na litakuwa la 19 katika historia ya mchezo huo.

Mara kwa mara Roger Federer na Novak Djokovic wamekuwa wakiingia katika hatua hiyo kwa kipindi cha misimu 11, hivyo hii ni mara ya kwanza kumuacha Nadal akiendelea hatua inayofuata.

Katika mchezo wa nusu fainali Nadal anatarajia kukutana na bingwa namba 24 kwa ubora duniani Matteo Berrettini raia wa nchini Italia ambaye ana umri wa miaka 23. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo.

Berrettini atakuwa nyota wa kwanza wa mchezo wa tenisi kutoka nchini Italia kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwenye US Open nchini New York ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1977.

Berrettini alifanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kumchapa mpinzani wake Gael Monfils ambaye anashika nafasi ya 13 kwa ubora wa mchezo huo. Berrettini alishinda kwa seti 3-6, 6-3, 6-2, 3-6, 7-6, juzi.

Nyota wengine ambao watapambana kwenye nusu fainali ni pamoja na Daniil Medvedev ambaye anashika nafasi ya tano kwa ubora kwenye mchezo huo ambaye anatokea nchini Urusi pamoja na Grigor Dimitrov anayeshika nafasi ya 78 kutoka nchini Bulgaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles