27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Lloris aitoa Tottenham ubingwa England

LONDON, ENGLAND

MLINDA mlango wa Totteham, Hugo Lloris, ameweka wazi kuwa timu hiyo haiwezi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, kikubwa wanatakiwa kupambana kuwania nasi ya pili kwenye msimamo.

Kipa huyo anaamini wakiweza kufanikiwa kuipigania nafasi ya pili na kufanikiwa mara kwa mara watakuwa na uwezo wa kuwania nafasi ya kwanza.

Tottenham msimu huu wamenza kwa kusuasua wakitoa sare dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City, Arsenal, wakifungwa dhidi ya Newcastle na kupata ushindi dhidi ya Aston Villa na kuwafanya Tottenham washike nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo minne.

Ligi hiyo ya England kwa sasa imesimama kupisha michezo ya timu za taifa iliyopo kwenye kalenda ya FIFA, hivyo Tottenham inatarajia kushuka dimbani Septemba 14. Lloris amedai wanahitaji muda kuifanya timu hiyo iwe kinara wa Ligi.

“Timu ya Manchester City na Liverpool wana wachezaji wengi ambao wana uzoefu wa hali ya juu, hizi ni timu ambazo zina ushindani wa hali ya juu.

“Ninadhani kwa kipindi hiki kuna baadhi ya vitu tunavikosa, lakini tutaangalia hapo baadae inawezekana mambo yakabadilika kwa kuwa soka ndivyo lilivyo.

“Kitu muhimu kwetu kwa sasa ni kuangalia jinsi gani tunatakiwa kukifanya ili kuhakikisha tunapata pointi katika kila mchezo ndani ya Ligi Kuu. Hivyo hadi kufikia Machi na April tutakuwa wapi kwenye msimamo wa Ligi.

“Tunajua ushindani ni mkubwa sana, lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya kutimiza malengo yetu. Kushika nafasi ya kwanza sio kazi ndogo, ila tuna uwezo mkubwa wa kupigania nafasi ya pili na hapo baadae tunaweza kupambana kwa ajili ya kuwania ubingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles