23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta: Tunamaliza kazi mapema tu

Mohamed Kassara -Dar es salaam

NAHODHA wa timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema kuwa baada ya kupata sare ya bao 1-1 na Burundi ugenini katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia, wanajipanga kumaliza shughuli iliyobaki nyumbani.

Stars ililazimisha sare hiyo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Inwari, jijini Bujumbura.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa juzi, Samatta alisema wamefurahishwa na matokeo waliyoyapata, hivyo watajipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa marudiano nyumbani na kusonga mbele.

Alisema matokeo waliyopata siyo mabaya na kwamba sare hiyo haiwapi nafasi ya kujiona wamemaliza kazi, badala yake wanatakiwa kukaza buti katika mchezo wa marudiano.

“Tumefurahishwa na matokeo tuliyopata, kwa wanaojua mpira wanafahamu umuhimu wa sare hii, hata hivyo tunarudi kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha tunamaliza shughuli mapema katika mchezo wa marudiano.

“Tunajua Burundi ni timu nzuri, lakini tukiwa nyumbani lolote linaweza kutokea, tunawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kutupa morali zaidi ya kupambana,” alisema mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles