Radi yaua watu 80 India

0
857

NEW DELHI, INDIA

WATU 80 wamefariki dunia nchini India baada ya kupigwa na radi katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa nchi ndani ya saa 24 juzi.

Kati ya hao, watu 53 walifariki dunia katika Jimbo la Bihar, 10 katika Jimbo la Mashariki la Jharkhand na  wengine 16 katika eneo la Madhya Pradesh.

Kwa mujibu wa maofisa nchini hapa, wengi wao walifariki wakiwa bado wanafanya kazi katika mashamba yao, ikiwa ni msimu wa mvua.

Katika muongo uliopita, zaidi ya watu 2,000 walifariki dunia kwa kupigwa na radi nchini hapa.

Ni vigumu kubashiri lini janga la radi litatokea na si rahisi kwa utawala kutoa tahadhari ya kutokea kwa radi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here