24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yaendeleza ukaidi, yarusha makombora

Joeng Joon-heeSEOUL, KOREA KUSINI

KOREA Kaskazini kwa mara nyingine jana inadaiwa kufanyia majaribio makombora yake mawili ya nyuklia, ikiwa ni dharau ya wazi kwa Umoja wa Mataifa (UN) ulioliwekea taifa hilo vikwazo vya kiuchumi.

Taarifa zinasema kombora la kwanza halikufanikiwa, huku la pili likisafiri umbali wa kilomita 400.

Msemaji wa Waziri wa Umoja wa Kitaifa wa Korea Kusini, Joeng Joon-hee, amesema majaribio hayo ni ukiukaji wa dhahiri wa vikwazo vya kimataifa.

“Ulipuaji huo makombora kwa kutumia teknolojia ya angani, unakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. Ni uchokozi dhidi yetu.

“Tunashauri ni vyema kwa Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani eneo la rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambao Korea Kaskazini imekuwa ikisititiza kila wakati,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amelaani hatua hiyo ya Korea ya Kaskazini.

“Leo (jana) kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika zamani, huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hatutaruhusu hili lipite bila kuchukua hatua, tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo,” alisema Abe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles