25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pwani wapigia debe uwezeshaji wa Benki ya Maendeleo

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAA

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amepongeza uwekezaji uliofanywa na Benki ya Maendeleo TIB katika kuchagiza Pwani ya Viwanda kwa kutoa mikopo katika miradi yenye tija na maendeleo mkoani humo.

Hayo aliyasema jana wakati alipotembelea kushuhudia miradi iliyowezeshwa na benki hiyo wakati wa maonesho ya wiki ya viwanda ayaliyokuwa yakifanyika mkoani humo.

Alisema kuwa uwekezaji huo wa TIB umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha shughuli za uwekezaji katika viwanda. 

“Tumeshuhudia uwekezaji wa Benki ya Maendeleo TIB ulivyoleta manufaa mkoani kwetu hali inayochagiza shughuli za maendeleo hasa katika kutoa ajira mkoani Pwani,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa uwepo wa Benki ya Maendeleo TIB mkoani Pwani kumechangia kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa vitendo lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya kuchagiza Tanzania ya Viwanda.

Aliongeza kuwa Benki ya Maendeleo TIB imekuwa sehemu muhimu ya utekelezaji kwa uchumi wa viwanda kwa kuwa kichocheo cha kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi hususani kwenye maeneo yenye viwango hatarishi vikubwa.

Aliyataja mafanikio yaliyoletwa na uwekezaji wa benki hiyo ikiwemo uwezeshaji wa kampuni ya uzalishaji kuku ya Mkuza na Kampuni ya Vifungashio ya Global zilizopo mkoani Pwani.

“Tunawashukuru sana TIB kwa kuwawezesha watu wa sekta binafsi ambao kwa hakika tunawashuhudia wanavyofanya vizuri mkoani kwetu,” alisema

Alisema “Ijenge Tanzania Wekeza Pwani Mahali Sahihi kwa Uwekezaji” unachagizwa na utekelezaji wa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inalenga ukuzaji wa sekta ya viwanda.  Hivyo, TIB kama benki ya kisera ina mchango mkubwa katika kufadhili miradi ya kimkakati katika kuendeleza viwanda hapa nchini.

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo ambao wako mkoani Pwani walisema kuwa mikopo iliyotolewa na Benki ya Maendeleo TIB imewezesha kuongeza tija na uzalishaji hali inayochangia kuongeza uwekezaji na kutoa ajira kwa Watanzania.

Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mkuza, Doreen Maximambali alisema kuwa mkopo uliotolewa na Benki ya Maendeleo imewezesha kubadilisha mfumo wa uzalishaji kutoka uzalishaji wa mikono hadi uzalishaji wa kutumia mitambo inayojiendeshea yenyewe.

“Mkopo wa TIB umewezesha kuboresha utendaji kazi wetu kwa kuongeza uzalishaji kwa kutumia mitambo inayojiendeshea yenyewe hali inayochangia kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje,” alisema.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles