27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

PUMA YAJA NA MRADI WA ‘SKY IS THE LIMIT’

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), imezindua mradi unaojulikana kama ‘Sky is the Limit’ wenye lengo la kuwatambulisha na kuwapa uelewa wanafunzi wa shule za msingi kuhusu masuala ya anga.

Meneja Masoko wa Mafuta ya Ndege Tanzania kutoka Kampuni ya Puma, Illuminata Yateri, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa mradi huo unataka kuamsha moyo wa ujasiri na kujiwekea malengo kuhusu jinsi ya kufanikiwa.

“Lengo la mradi huo ni kuwahamasisha watoto wanaotoka katika mazingira ya kawaida sana ya vijijini kwa kuwatia moyo katika masomo yao ili wajue na kuvutiwa na sekta ya anga na maeneo mengine ya fursa za kazi za nje ya maeneo wanaoishi.

“Katika kufanikisha mradi huo zaidi ya wanafunzi 40 kutoka Shule za msingi za wilayani Kisarawe wamepata fursa ya kutembelea Shirika la Ndege la Air Tanzania pamoja na kushuhudia namna Kampuni ya mafuta ya Puma inavyohifadhi mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam,” amesema.

Amesema mradi huo wa Sky is the limit utawapa watoto kutoka shule za msingi waliochaguliwa kutoka kwa jumuiya zisizo na fursa na uzoefu wa sekta ya anga kwa ukaribu zaidi, kwa kufanya ziara ya elimu inayofanywa katika miundombinu ya uwanja wa ndege kama ugavi wa mafuta ya ndege, huduma zinazotolewa kwenye ndege, udhibiti wa safari za ndege, kupata habari mbalimbali za ndege kupitia watalaamu wa sekta hiyo.

“Watoto watajua shughuli za kampuni ya mafuta ya Puma kuhusu biashara ya mafuta ya ndege jinsi yanavyouzwa kwenye ndege za ndani na za kimataifa.

“Tunashukuru mamlaka ya Kisarawe chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo, Ofisa Elimu Wilaya ya Kisarawe pamoja na walimu husika kwa msaada wa kupata wanafunzi hawa ambao leo hii wamejifunza kwa vitendo,” amesema Yateri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles