27.8 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Magufuli: nimefunga mnada wa korosho, tutazinunua wenyewe

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amefunga mnada wa korosho kwa kuzitaka kampuni zilizotaka kuzinunua kusitisha uamuzi huo kwani serikali itazinunua zote kwa bei elekezi ya Sh 3,000 kwa kilo moja.

Aidha, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuzielekeza kampuni zote zilizojaribu kuleta mapendekezo kwake kwa ajili ya kununua korosho hizo kusitisha zoezi hilo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua Jumamosi wiki iliyopita.

“Waambie waache, watakuja kutuchezea watakwambia wanataka tani 200,000 lakini baadaye wataanza kutuleteza masharti, wamesema watanunua kwa bei elekezi Sh 3,000 je, ikipanda Desemba?

“Kwa hiyo wanaokuja waambie waache sasa ni saa 5:12, nimeshafunga wala wasije korosho tutanunua wenyewe.

“Nimepiga hesabu mimi si mchumi korosho iliyobanguliwa ni kati ya Sh 3,000 na korosho ambazo zinategemewa kupatikana mwaka huu ni tani zaidi ya laki mbili,” amesema.

 

 

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,383FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles