24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mkenda amlilia Mramba

Na Upendo Mosha,Moshi

Mbunge wa Jimbo Rombo, mkoani Kilimanjaro, Profesa Adolf Mkenda, amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na kwamba atamkumbuka kama kiongozi shupavu, mvumilivu na muungwana.

Basil Mramba enzi za Uhai wake akiwa Waziri wa Fedha.

Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Kilimo nchini, ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 17, 2021 baada ya kupokea taarifa za kifo cha Mramba aliyefariki leo katika hospitali ya Regency Dar es Salaam.

Amesema kifo cha Mramba kimekuwa ni pigo kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo kutokana na kwamba alikuwa kiongozi shupavu, mwenye busara, mvumilivu na muungwana.

“Historia ya maisha, wasifu na haiba yake vilitosha kumfanya kuwa ni kiongozi wa kutegemewa na sisi sote hata baada ya kuondoka kwenye siasa, alikuwa mbunge wa Rombo kwa miaka 20 alitumia nafasi yake kujenga na kueendeleza jimbo letu,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema Mramba ambaye alikuwa waziri katika wizara mbalimbali atakumbukwa katika utumishi uliotukuka ikiwemo juhudi alizozifanya katika kuimarisha mazingira ya kibiashara na uwekezaji.

“Pamoja na kufanya mambo mengi, kubwa tutakalomkumbuka nalo Mramba akiwa waziri wa fedha ni namna alivyo ondoa tozo nyingi ambazo zilikuwa kero katika uchumi wetu,”amesema Prof. Mkenda.

Ameongeza kuwa licha ya madhila aliyokuwa akiyapitia Mramba baada ya kuondoka katika nafasi ya ubunge hakuwa na kinyongo na aliendelea kupigania maendeleo ya wananchi jimboni humo.

“Rombo na Taifa letu tumempoteza mtu ambaye alikuwa mahiri kwani baada ya kukosa ubunge bado hakuwa na kinyongo alikuwa mcheshi na aliendelea kupigania maendeleo ya jimbo na Taifa letu hivyo natoa pole nyingi kwa Mjane wa marehemu, watoto ndugu jamaa na marafiki,” amesema Profesa Mkenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles