26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. MUHONGO AJADILI UFAULU MBAYA WA WANAFUNZI JIMBONI

musoma

Na SHOMARI BINDA

KUSHUKA kiwango cha elimu na  matokeo mabaya kwa shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, kumesababisha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kukutana na walimu wakuu na waratibu elimu kusaka ufumbuzi.

Katika kikao hicho cha tathimini kilichofanyika Kata ya Mugango, baadhi ya walimu wakuu walieleza changamoto zinazosababisha kufanya vibaya na kushika nafasi za mwisho ngazi ya mkoa kwa shule zao kuwa ni upungufu wa walimu na ubovu wa miundombinu.

Mwalimu Michael Warioba kutoka Shule ya Msungi Chitare, alisema upungufu wa walimu ndiyo kikwazo kikubwa sana kwao kufanya vibaya.

Alisema  shule 111 zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu.

Alisema ili kupata matokeo na ufaulu mzuri upungufu wa walimu unapaswa kuangaliwa na kusisitiza kuwa kuna baadhi ya shule zenye wanafunzi zaidi ya 800 lakini  zikiwa na walimu watano tu hali ambayo haiwezi kutoa  matokeo mazuri.

Mwalimu mwingine alisema kipindi kiliochopita kulikuwa na upungufu mkubwa wa vitabu vya kufundishia lakini kwa sasa wamepokea msaada wa vitabu zaidi ya 40000 hivyo imani yao ni kwamba vitasaidia kuwaongezea ufaulu ingawa bado changamoto ya walimu ipo.

“Tunakushukuru Mbunge kwa msaada wa vitabu ulivyotoa, sasa tukipata na walimu wa kutosha imani yetu hali itabadilika sana na kufanya vizuri kwenye matokeo yajayo,”alisema.

Akizungumza kwenye kikao hicho,   Profesa  Muhongo, alisema kwa kuwa kipaumbele chake ni elimu atahakikisha   anashirikiana na wadau   na serikali kuweza kuzitatua ili kupata matokeo mazuri.

Alisema shule tatu zitakazofanya vizuri kwenye halmashauri na ngazi ya mkoa zitapata zawadi kutoka kwake.

Mbunge huyo alisema  kikao cha kutathimini matokeo ya mwaka 2018 kitafanyika wiki moja baada ya matokeo na washindi kupata zawadi zao.

Hivyo aliwaomba walimu kuweka malengo kwenye shule zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles