25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mbarawa asisitiza matokeo kwenye usafiri wa Reli

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha inaisimamia Menejimenti kwenye eneo la uendeshaji ili kuboresha utoaji wa huduma hususani kwa wasafirishaji wa mizigo.

Prof. Makame Mbarawa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023 wakati akizindua bodi hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema ufanisi katika huduma za reli utaongeza mzigo na kulifanya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida.

“Kwenye eneo la ujenzi mnakwenda vizuri lakini bado kwenye uendeshaji hakuna utendaji mzuri, leo wasafirishaji wana mzigo wa kutosha lakini wakija kutafuta mabehewa wanaambiwa wakae foleni, hii haiwezekani kuendelea namna hii, Mwenyekiti simamia hili’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameeleza umuhimu wa matumizi ya tiketi mtandao kwa abiria na kuitaka TRC kuboresha mifumo ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa abiria wanaolazimika kukaa muda mrefu kusubiria kukata tiketi wanapotaka kusafiri.

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha reli zote mbili zinakuwa na tija hivyo ameitaka TRC kuchukua hatua stahiki kwa kutafuta wabia watakaoendesha treni maraa baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali itaendelea kuhakikisha fedha inazotenga kwenye bajeti za kila mwaka zinatumika katika kuboresha shirika hilo ambalo bado linahitaji vitendea kazi ili kujiendesha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ally Amani amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi imejipanga kutumia uzoefu ulionao kuhakikisha shirika hilo linakuwa na tija na kujiendesha kwa faida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles