28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

PREZZO AFUTA ‘TATTOO’ YA MICHELLE

NAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Jackson Makini, maarufu kwa jina la Prezzo, amefuta picha ya aliyekuwa mpenzi wake Michelle Yola.

Prezzo na Michelle walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka miwili na nusu, katika kipindi hicho kila mmoja alichora picha ya mwenzake kwenye mkono, lakini baada ya wawili hao kuachana miezi michache iliyopita Prezzo ameamua kufuta mchoro huo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Prezzo aliposti video ikimuonesha anaifuta picha hiyo huku akisema kwamba huo ndio mwisho wa kumkumbuka Michelle.

“Kama kuna kitu chochote kitatokea kwangu basi ni mimi mwenyewe, naifuta tattoo hii nikimaanisha kwamba Michelle aniache na maisha yangu kama nilivyomwacha yeye,” alisema Prezzo.

Hata hivyo, Michelle alitumia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa, anaendelea na maisha yake na hana mpango wa kumsikia Prezzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles