28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

AMBER ROSE: NATAKA KUOLEWA NA 21 SAVAGE

NEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Amber Rose, amefunguka na kusema yupo kwenye mipango ya kutaka kuolewa na rapa Shayaa Joseph anayejulikana kwa jina la 21 Savage.

Amber mwenye umri wa miaka 33, amesema mipango hiyo ya kutaka kuolewa na msanii huyo mwenye umri wa miaka 24 inaendelea kufanyika na tarehe rasmi itatangazwa.

“Nadhani sasa nipo sehemu sahihi kwa 21 Savage, ananifanya niwasahau wanaume wengine katika maisha yangu, siwezi kumsahau Wizkhalifa kwa kuwa ni baba wa mwanangu, lakini siwezi kumwelezea chochote kwa sasa.

“Kitu ambacho naweza kukizungumzia ni juu ya uhusiano wangu na 21 Savage, kilichopo kwa sasa ni juu ya kuja kuoana, nadhani kila kitu kitawekwa wazi kwa kuwa mambo ni mazuri,” alisema Amber.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles