27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAKINI APAMBANA KUJITANGAZA KIMATAIFA

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kundi la Weusi, John Makini, amesema mipango yake ni kuhakikisha anafanya  kazi bora zaidi zitakazoweza kumtangaza kimataifa.

Makini ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Kata Leta’ aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Davido, alisema ili msanii aweze kufanikiwa lazima ajitangaze kwa kufanya kazi zenye ubora.

Alisema tasnia nzima ya muziki kwa sasa imeonyesha ushindani wa hali ya juu, si kwa wasanii Watanzania tu hata wale wa nje ya nchi.

“Mipango yangu ni kufanya kazi bora zaidi na zaidi, hivyo mara baada ya kuachia ‘Kata Leta’ kazi nyingine kali itafuata.

“Nimegundua ili uweze kujitangaza lazima uvuke mipaka ya Tanzania, kutafuta wasanii wakubwa wa kimataifa ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuwashirikisha kwenye kazi zako,” alisema Makini.

Msanii huyo hadi sasa amefanikiwa kuwashirikisha wasanii watatu wa kimataifa  katika kazi zake tofauti ambao ni Chidinma na Aka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles