VATICAN CITY, VATICAN
POLISI wa Vatican wamemkamata padre, ambaye ni mwanadiplomasia wa zamani wa Ofisi ya Papa katika Ubalozi wa Marekani, akishukiwa kumiliki picha za ngono za watoto.
Mwanadiplomasia huyo, Carlo Alberto Capella alikamatwa baada ya uchunguzi.
Capella aliondoshwa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini hapa Septemba 2017, baada ya taifa hilo kuiambia Vatican uwezekano wa ukiukaji wa picha za ngono za watoto kulikofanywa na mmoja wa wanadiplomasia wake.
Alipata daraja la upadre mwaka 1993 na kujiunga katika jopo la wanadiplomasia wa Vatican mwaka 2004.
Kukamatwa kwake kunaweza kuibua upya juhudi za Papa Pope Francis kukomesha vitendo vya udhalilishaji watoto katika Kanisa la Katoliki.
Aliahidi kutovumilia vitendo kama hivyo, lakini wakosoaji wake wanasema hajafanya vya kutosha kuwachukulia hatua maaskofu wanaodaiwa kufumbia macho ukiukaji huo.