27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi: Hamza alikuwa gaidi

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

UCHUNGUZI wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa Hamza Mohammed aliyewaua kwa risasi watu wanne, wakiwamo polisi, alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu, baada ya kuwaua kwa risasi polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi iliyoko jirani na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Septemba 2, 2021, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura, amesema uchunguzi uliofanywa na polisi umebaini Hamza aligubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

Amesema alikuwa akijifunza mambo ya kigaidi kupitia mitandao ya kijamii, ambapo kwa kipindi kirefu amekuwa akifuatilia mitandao inayoonesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS.

Ameongeza kuwa taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia polisi kwa sababu walimdhulumu madini yake si za kweli kwani hakuwa na madini wala fedha na umiliki wake wa mgodi wa dhahabu Chunya ulisimama kwa muda mrefu.

“Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini Chunya. Uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwishasimama muda mrefu,” amesema Wambura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles