23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia: Tozo zitaendelea,tutajenga madarasa 500

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema tozo za miamala ya simu zitaendelea kuwepo na hataki kudanganya kuwa zitaondolewa, huku akisema za Septemba na Oktoba kujenga madarasa 500.

Rais amezungumza hayo leo Alhamisi Septemba 2, wakati aliposimama njiani katika eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam akielekea Bagamoyo kurekodi kipindi maalum cha kutangaza utalii.

“Nataka niwaambie tozo zitaendelea kuwepo na sitaki kuwaficha kwa sababu tozo zile miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya bilioni 60 hivi na zimepelekwa kujenga vituo 220 vya afya, hivyo tunajenga wenyewe.

“Tunajitegemea wenyewe ili kuweka mkono kwa wafadhiri wanaokuja na masharti yao wasituingilie mambo yetu na ndivyo tutaweza kufanya wenyewe. Tuna mambo mengi ya kufanya, tuna miradi mikubwa tulioachiwa na Rais wetu Hayati Dk. Magufuli tunaendelea kuitekeleza na ninawaahidi tutaitekeleza kama ilivyopangwa,”amesema Rais Samia.

Ameeleza anajua akifanya kitu atasemwa  na asipofanya atasemwa, hivyo bora afanye na anachokifanya kitaonekana.

“Wanadamu ukifanya watasema, usipofanya watasema, bora tufanye waseme lakini wakione kuliko kutofanya kwa kuogopa maneno yao. Wanasema kelele za mlango hazimwachishi mwenye nyumba kulala sababu tumezizoea, kusemwa kupo.

“Kuna miradi ya kijamii kama shule, barabara na hospitali tunaendelea kuitekeleza, zamani tulikuwa tunasaidiwa na wahisani lakini sasa hivi wamebadilika, badala ya misaada wanakuja tufanye biashara, tugawane faida,”amesema

Ameeleza kuwa  alisikia kilio cha Wanachini na kukaa na wataalamu na kupunguza asilimia 30 ya tozo, tofauti na  iliyopitishwa katika bajeti.

Rais Samia amesema fedha zitakazikusanywa Septemba na Oktoba, zitatumika kujenga madarasa 500 Tanzania nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles