‘Ufaza’ wamponza Ziyech

0
22120

KOCHA wa timu ya taifa ya Morocco, Vahid Halilhodzic, amesema Hakim Ziyech amekuwa na tabia za kujiona ndiye mfalme kikosini na ndiyo maana hakumwita kwenye mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Licha ya Halilhodzic kutowaita Adel Taarabt na Sofian Boufal, wengi walishangaa kuona akienda kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia bila huduma ya Ziyech.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Halilhodzic amesema Ziyech anayeichezea Chelsea ya Ligi Kuu ya England amekuwa na vitendo vya utovu wa nidhamu.

“Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu ya soka, nimeona mchezaji asiyetaka kufanya mazoezi akijifanya ni majeruhi, huku vipimo vikionesha si kweli,” ameongeza kocha huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here