22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Polepole kutoa bajaji 10 Iringa

RAYMOND MINJA – IRINGA

Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi( CCM ) Hamprey
Polepole, ameahidi kutoa bajaji kumi kwa umoja wa madereva bajaji Mkoa wa Iringa ili ziweze kuwasaidia kujikwamua kiuchumi .

Ametoa ahadi hiyo leo Juni 10 wakati wa ufunguzi wa tawi la madereva la Mwembetogwa ikiwa ni pamoja na kuwakabithi rasmi kadi za chama hicho jumla ya madereva 300 wa tawi hilo ambapo amesema kuwa CCM ni chama kinachofanya kazi kwa vitendo hivyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi watatoa bajaji kumi ili ziweze kuwasaidia vijana kujikwamu kiuchumi .

“Nimekuja hapa leo kufungua tawi lenu hili lakini nimesikia
risala yenu kuwa kuwa mnahitaji bajaji na viwanja na chama hiki sio
cha porojo tunafanya kazi kwa vitendo sasa mwenyekiti wa wilaya
hizi kadi usitoe leo bali uzitoe Julai 20 ukiambatanisha na
bajaji kumi ili ziwasaidie vijana wetu hawa wanaomuunga mkono Rais
wetu John Magufuli”

“Ndugu zangu mlisema mnahitaji viwanja au kauli kwa tasisi za fedha
ili muweze kukopeshwa fedha kwa kuwa hamna dhamana sasa hizi bajaji
kumi zikawe ni dhamana kwenu ili sasa muweze kufanya kazi na kuongeza bajaji nyingine ili sasa vile viwanja mlivyoomba mvipate kwa kutumia bajaji hizi “

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubea
amesema kuwa chama hicho kimejipanga kusikiliza na kutatua kero kwa
wanachi wake hivyo kwakuwa wamefanikiwa kuwafikia watu wote hasa wale wa ngazi ya chini wanaamini uchaguzi unaokuja watashinda kwa kishindo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles