30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Shahidi kesi ya Malinzi adai fedha za udhamini zilitumika bila nyaraka za uthibitisho

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mkaguzi wa Ndani wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Richard Magongo, amedai baadhi ya fedha zilizotolewa na TBL kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa ajili ya kudhamini timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ zilitumika bila kuwa na nyaraka za uthibitisho wa matumizi.

Magongo amedai hayo leo Juni 10 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde,  wakati akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai.

Alidai TBL iliingia katika mkataba na hilo wa kuidhamini Taifa Stars mwaka 2012 kwa miaka mitano ambapo jumla fedha za udhamini zilikuwa Dola za Marekani, 10,000,000.

Shahidi anadai walikuwa wakifanya ukaguzi wa fedha hizo kila inapofika robo mwaka na taarifa za ukaguzi zilibainisha kwamba fedha za udhamini zilitumika bila kuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi, kulikuwa na matumizi ambayo hayakuwa ndani ya mkataba na mapungufu yalikuwa mengi kiuhasibu na kiutawala kwa TFF katika utekelezaji wa mkataba.

“Matumizi ambayo hayakuwa na nyaraka za uthibitisho ni mengi, mfano marejesho ya mikopo kwa Jamal Malinzi hayakuwa na nyaraka za kuonyesha lini aliikopesha TFF.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles