33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Pogba awaomba radhi Man United

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba, amewaomba radhi mashabiki wa Manchester United baada ya juzi kusababisha penalti na timu yake kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Kiungo huyo aliweka wazi kuwa, hana uwezo mkubwa wa kucheza kama mkabaji, hivyo kutokana na hali hiyo alijikuta akifanya makosa kwenye eneo la hatari na kuwapa wapinzani zawadi ya penalti iliyowekwa wavuni na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Aubameyang katika dakika ya 69 kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu nchini England.

Manchester United walikubali kichapo hicho huku wakitoka kwenye kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya RB Leipzig katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki moja iliopita.

Hata hivyo, Pogba raia wa nchini Ufaransa alisema, mbali na kupoteza mchezo huo, lakini timu yake haikuwa kwenye kiwango kizuri na ndio maana walipoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani.

“Baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig, timu bora imeshindwa kufanya hivyo tena, lazima tuangalia kwa nini imetokea hivyo, kwa upande wangu nimefanya kosa ambalo limelata madhara kwa timu, sikutakiwa kufanya kosa kama lile kwenye eneo la hatari, kikubwa nilitakiwa kuucheza mpira tu, lakini baada ya kufanya hivyo nikasababisha kupoteza mchezo huo.

“Tulitakiwa kuwa bora na kufunga mabao kwenye mchezo huo, kwa upande wangu nilitakiwa kuwa bora zaidi, nimefanya kosa la kijinga sana, hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba radhi Man United kwa kile kilichotokea,” alisema Pogba.

Kutokana na matokeo hayo, Manchester United wamebaki nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi huku wakiwa na jumla ya pointi saba baada ya kucheza michezo sita, wakati huo Arsenal wakiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo saba na kuvuna pointi 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles