27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Lewis Hamilton kustaafu Formula One

BOLOGNA, ITALIA

NYOTA wa mbio za magari duniani, Lewis Hamilton, amedai kuwa anafikiria kuachana na Formula One mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Bingwa huo wa magari raia wa nchini Uingereza, ametoa kauli yake hiyo baada ya kupata ushindi katika mashindano ya Emilia Romagna Grand Prix na kukaribia kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa dunia mara saba.

Iwapo atafanikiwa kushinda katika hatua nyingine ya mashindano hayo mjini Istanbul, Uturuki Jumapili hii, atatawazwa kuwa bingwa bila kujali kiwango kitakachoonyeshwa na mpinzani wake, Valtteri Bottas.

Alipoulizwa wasiwasi juu ya bosi wake, Toto Wolff, Mtaliano mwenye umri wa miaka 48, anayefikiria kumpa nafasi ya Mwenyekiti au Mkurugenzi Mkuu wa Fomular One, Hamilton alisema, “Kwanza wala sifahamu iwapo nitaendelea kuwa hapa mwakani, hivyo hilo halinihusu kwa sasa.

“Toto na mimi, tumekuwa na mazungumzo mengi ya kina na ninafahamu anafikiria nini. Tulikabiliana na mengi kwa pamoja.Nimekuwapo hapa kwa muda mrefu, muda mrefu sana na ninaweza kuelewa anataka kupunguza baadhi ya mambo na kutumia muda mwingi na familia yake.

“Sifahamu ni nani atakayechukua nafasi yake lakini yeye ni kiongozi na hawezi kumweka mtu katika nafasi yake ambaye hataweza kuifanya kazi yake ipasavyo. Atatafuta mtu sahihi.”

Akizungumzia mbio hizo za msimu wa 17, Hamilton mwenye umri wa miaka 35, aliongeza: “Kwa sasa tupo Novemba na Krismasi haipo mbali. Ninajisikia furaha kubwa, nina nguvyu na nitaendelea kuwa fiti kwa miezi kadhaa ijayo, lakini Toto alizungumzia suala hilo na kuna mambo mengi kichwani mwangu.

“Ningependa kuwapo hapa mwakani lakini hakuna uhakika juu ya hilo. Kuna mambo mengi yanayonivutia kuhusiana na maisha yangu baada ya F1, hivyo muda utaongea.”

Kumekuwa na shaka iwapo ni kweli Hamilton anamaanisha juu ya kustaafu kwake kwani kwa siku za hivi karibuni, amekuwa akizungumzia juu ya mpango wake wa kuendelea na mbio hizo.

Kwa upande mwingine, inadhaniwa kuwa kauli yake hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa tetesi kwamba amefanya makubaliano ya kulipwa pauni milioni 40 kwa mwaka na kampuni ya Mercedes.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles