27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Pochettino: Sikutarajia Messi kuja PSG

KOCHA wa PSG, Mauricio Pochettino, amesema usajili wa Lionel Messi klabuni hapo ulimwacha mdomo wazi kwa kuwa hakuutarajia.

“Sikudhani kama ingewezekana (Messi kutua PSG)… Nimekuwa nikivutiwa naye kwa muda mrefu, tangu nilipokuwa nakutana naye kama mpinzani. Kwa hiyo, ni jambo zuri sana kuwa naye mazoezini. Nafikiri tukiwa pamoja tutafikia ndoto ya klabu.”

Messi (34), aliondoka Barca wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka huu, na hiyo ilitokana na ukata unaoiyumbisha klabu kongwe hiyo katika historia ya Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Ukimlinganisha na Pochettino, si tu wote ni Waargentina, bali pia wawili hao ni mashabiki wakubwa wa klabu ya nchini kwao, Newell’s Old Boys, huku wakiwa ni wazawa wa Mji mmoja; Rosario.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles