33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Sitaki mazoea Yanga

PluijmNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van der Pluijm, amesema hataki kuwa na kikosi cha mazoea, hivyo wachezaji atakaowatema wanatakiwa kujifunza na kujifua upya ili aweze kuwarudisha tena kuitumikia klabu hiyo kipindi cha dirisha dogo.
Wachezaji wazawa wanaotajwa kupitiwa na panga la kuachwa ni Jerryson Tegete, Danny Mrwanda, Husein Javu, Said Bahanuzi, Nizar Khalfan, Omega Seme, Alphonce Matogo na Hamis Thabiti.
Pia huenda ikawatema wachezaji wake wa kigeni, Andrey Coutinho na Kpah Sherman, huku nafasi zao zikitarajiwa kuzibwa na wachezaji kutoka Zimbabwe, Mmali Kamara na Donald Ngoma, wakati wanaotarajiwa kufanyiwa majaribio ni James Abban na mshambuliaji, Daniel Darkwah kutoka Ghana.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm ambaye yupo likizo nchini Ghana alisema kila mchezaji aliyeachwa ana mapungufu ambayo anaweza kuyarekebisha na kupata nafasi kuichezea Yanga tena.
Mholanzi huyo alisema, kuendelea kubeba wachezaji wasiokuwa na sifa, kunachangia kumaliza viwango vyao ambavyo viliwapa nafasi ya kuchaguliwa katika timu hiyo.
“Hakuna haja ya kuendelea kubeba kikosi kwa mazoea kisa mchezaji ameichezea timu muda mrefu na huko nyuma alikuwa vizuri sasa hayupo sawa, tuendelee kuvumilia kwa matumaini ya kuona mabadiliko mbele.
“Wachezaji wote ambao nimeamua kuwaacha wana viwango, ila wanahitaji kujifua zaidi nje ya Yanga hapo labda wanaweza kuonyesha mabadiliko yatakayonivutia kuwaita tena,” alisema Pluijm.
Pluijm ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo, alisema endapo wachezaji waliotemwa watabadilika ataweza kuwafikiria wakati wa usajili dirisha dogo.
Kocha alieleza anatambua maamuzi yake yanaweza kupingwa na wengi, lakini amelenga kuitengeneza Yanga yenye kikosi bora na siyo bora kikosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles