28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii kusaka historia mpya Tuzo za Kili, Juni 13

linahWanagombea tuzo sitaNA MWANDISHI WETU
WAKATI washindi wa vipengele mbalimbali katika tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2015 (KTMA) wakitarajiwa kujulikana Juni 13 katika hafla ya ugawaji wa tuzo hizo, hakuna msanii atakayevunja rekodi ya Abdul Nassib (Diamond) kwa kuwa hakuna aliyeko katika vipengele saba.
Tuzo hizo zilizoanza mwaka 2000 hadi leo zina rekodi iliyowekwa na Diamond ya kunyakua tuzo saba mwaka jana, mwaka huu amekutana na mchuano mkali baada ya kuingia katika vipengele sita akichuana na Ali Kiba na Juma Jux ambao nao wanataka kuweka rekodi ya kihistoria ya kunyakua tuzo nyingi katika shindano hilo.
Mbali na Diamond kuvunja rekodi msimu uliopita, Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa pia iliwahi kunyakua tuzo tano mwaka 2013, huku wasanii, Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakinyakua tuzo tatu kila mmoja.
Kwa mwaka huu katika shindano hilo lililopo chini ya udhamini wa Kampuni ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro, yanaonyesha kuvutia hiyo rekodi mpya itakayoshindanisha wasanii hao wa Bongo Fleva ambao wanatamba kuwa na mashabiki wengi kwa sasa.
Pia wasanii wa muziki wa aina nyingine ukiwemo taarabu na nyimbo za asili huwa zikinyakua tuzo nyingi kutokana na muziki wao kuwa na mvuto mkubwa kwa ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Kurwijira Maregesi, zoezi rasmi la upigwaji wa kura litafungwa Juni 5 baada ya kufunguliwa Mei 4 na mwaka huu hivyo kila msanii aliyepo katika kipengele chochote awashawishi mashabiki wake wampigie kura zaidi wawezavyo ili aibuke mshindi.
Basata mwaka huu wameendelea kusimamia vema uchaguzi wa nyimbo kwa kufuata maudhui ya wimbo huku wakiachana na nyimbo zenye maneno yasiyo na mafunzo zaidi ya kutumia tafsida kuhalalisha lugha chafu.
Mwaka jana ilizuia wimbo wa Jux na Snura Majanga kutokana na kutokuwa na kukiuka maadili katika video za nyimbo zao na mwaka huu wamefanya hivyo kwa nyimbo zisizostahili ubaya uko wapi?
Jux aliyezuiwa wimbo wake mwaka jana, mwaka huu ameingia katika vipengele sita, hayo ni mabadiliko inaonyesha amekubali makosa yake na ameyafanyia kazi na sasa wananchi wanapiga kura kwa kutumia mfumo wa website ya www.ktma.co.tz, WhatsApp na njia ya SMS.
Tuzo hizi zinazosimamiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa muziki, kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa kuleta mageuzi katika fani ya muziki lakini pia zinatakiwa kufanyiwa marekebisho katika vipengele hivi; kwanza zitoe elimu zaidi ili ziondoe dhana potofu ya kuitwa mradi wa wachache ili baadhi ya wanaozisusia wasisuse ili ziongeze mvuto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles