26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Wemba kuzikwa Jumanne

Papa-WembaKINSHASA, CONGO

MWILI wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Papa Wemba, umewasili jana nchini humo ukitokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast alipofariki mwishoni mwa wiki iliyopita.

Msanii huyo alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.

Mwili wa msanii huyo tayari umewasili nchini kwao na kupokelewa na idadi kubwa ya watu katika uwanja wa ndege wa Kinshasa. Wengi wao walionekana wakiwa wamevaa nguo zenye picha yake huku zikiwa zimeandikwa ‘Kwaheri Papa Wemba’.

Mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya milele Jumanne ya wiki ijayo mara baada ya kuagwa siku ya Jumatatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles