Nape kuzindua siku ya madansa leo

NapeNA ESTHER MNYIKA

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, anatarajia kuzindua siku ya madansa duniani itakayoadhimishwa kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam leo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tanzania Disc Association (TMDA), Asanterabbi Mtaki, inaeleza kwamba  kwa mara ya kwanza madansa nchini wataungana na madansa wa mataifa  mengine duniani kuadhimisha siku hiyo inayoadhimishwa kila Aprili 29 ya kila mwaka.

“Lengo la maadhimisho hayo hapa nchini  ni kuhamasisha  madansa kushiriki, kujitolea kufanya shughuli za kijamii kivitendo na kuongeza uelewa ili wajitambue  kuwa ni sehemu  ya ajira ya kujipatia  kipato,” alieleza Mtaki.

Alisema baadhi ya madansa waliojitokeza kushiriki katika maadhimisho hayo ni Bombes group, Wakali Dancer, Athuman digadiga bingwa wa break-dance na funky Taifa pamoja na madj mbalimbali akiwemo Dj Seckklito, Dj john Peter Pantalakis, Dj disko na Dj Mafuvu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here