26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

P. Diddy kuachana na muziki

P-DiddyLOS ANGELES, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop, Sean Combs ‘P. Diddy’, ameweka wazi kwamba anatarajia kuachana na muziki na kujitupa kwenye filamu baada ya kuutumikia muziki kwa zaidi ya miaka 20.

Msanii huyo amesema anataka kuachia albamu yake ya mwisho ya muziki kisha kuingia kwenye filamu kwa asilimia 100, huku akiamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kibiashara.

“Natarajia kuachia albamu yangu ya mwisho kisha niingie kwenye filamu kwa asilimia 100, albamu yangu inaitwa ‘No Way Out 2’ hivyo nataka kuacha muziki katika mazingira mazuri na kuwa mshindi wa hip hop kwa kufanya maonyesho dunia nzima kwa mara ya mwisho,” alisema P. Diddy.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kudai kuachana na muziki, lakini wengi wanaamini kuwa safari hii itakuwa kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles