Operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul yaendelea

0
437

mosulMOSUL, IRAK

VIKOSI vya Irak vimeanza upya harakati za kuukomboa Mosul, mji pekee mkubwa unaodhibitiwa na wapiganaji wajiitao Dola la Kiislamu (IS) wakilenga sehemu ya mashariki ya Mto Tigris unaougawa mji huo.

Awali kikosi maalumu kinachopambana na ugaidi kilisitisha kwa muda opereshini zake wiki iliyopita baada ya kusonga mbele haraka kuliko vikosi vingine.

Mbinu hizo zililengwa zaidi kupunguza mwanya uliokuwepo na kuujongelea zaidi mji huo.

Vikosi vya usalama vya Irak na wanamgambo wa Kikurd wa Peshmerga wameanza operesheni zao Oktoba 17 wakisaidiwa angani na nchi kavu na ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.

Aidha wanamgambo wa madhehebu ya Shia wanaoungwa mkono na Iran wamejiunga na operesheni hizo Jumamosi iliyopit kwa lengo la kuifunga njia inayoiunganisha miji ya Mossul na Raqqa, ngome kuu ya IS nchini Syria.

Mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul wanakoishi watu milioni 1.5 yanaripotiwa kuwa makali zaidi katika kipindi chote cha vurugu kilichofuatia uvamizi wa Marekani uliomng’oa madarakani aliyekuwa kiongozi wa taifa hili Sadam Hussein  mwaka 2003.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here