25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Chama cha Democratic kiliteua mgombea asiyestahili-Pence

penceWASHINGTON, MAREKANI

MGOMBEA mwenza wa Donald Trump, Mike Pence amesema tangazo la Shirika la Upelelezi Marekani (FBI) kuhusu kashfa mpya za barua pepe zinazomhusu mgombea urais wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton ni ushahidi kuwa chama hicho kiliteua mgombea mwenye shaka.

Amesema hayo huku ikiwa imesalia takriban wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Marekani, ushindani mkubwa ukiwa kati ya Clinton na Trump wa Chama cha Republican.

Meneja wa kampeni wa Clinton John Podesta, hata hivyo ameliambia Shirika la Habari la CNN kuwa Mkurugenzi Mkuu wa FBI, James Comey, anapaswa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hatua yake ya kutoa tangazo tata siku chache kuelekea uchaguzi.

Lakini Pence amesisitiza kuwa sakata la barua pepe dhidi ya Clinton tangu mwanzo limekuwa na faida kwa kampeni zao na limewasogeza mbele.

Naye mgombea mwenza wa Clinton pia Tim Kaine, amebeza tangazo hilo la FBI na kusema halina maana yoyote.

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Marekani, kumekuwa na tambo nyingi kati ya wagombea hawa wawili ambapo, uamuzi kamili utafanywa na wapiga kura Novemba 8 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles