24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

NMB kuwakopesha wachimbaji wadogo zaidi ya Sh bilioni 120

Mwandishi Wetu

Benki ya NMB Plc imepanga kutumia zaidi ya Sh120 bilioni kutoa mikopo ya mitaji, vifaa na mitambo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika sekta ya madini nchini.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Klabu la Wachimba Madini kanda ya ziwa, (NMB Lake Zone Mining Club) Mkuu wa Idara ya Biashara kutoka makao makuu ya benki hiyo, Alex Mgeni alisema hadi sasa, tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh63 bilioni kwa kundi hilo.

“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na vifaa hivyo ndivyo vutakuwa dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo anaotaka kununua,” alisema Mgeni.

Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha wachimbaji kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uamuzi wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa sekta ya madini siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi wa wachimbaji na Taifa kwa ujumla.

“Teknolojia na mitaji ni kati ya changamoto sugu katika sekta ya madini, hasa kwa wachimbaji wadogo; benki ya NMB kutoa mikopo kutamaliza tatizo la mitaji na pengine litamaliza pia suala la teknolojia kwa sababu wachimbaji wataweza kuajiri wataalam na hatimaye kuchimba kwa tija,” alisema Bina

Huku akiwataka wachimbaji wadogo kuondoa hofu na dhana potofu kuhusu mikopo, Rais huyo wa Femata alizihakikishia taasisi za fedha fursa ya biashara ya mikopo katika sekta ya madini aliyosema yanaongezeka thamani hata katika kipindi hiki dunia inakabiliwa na janga la virusi vya corona.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel aliihakikishia NMB utayari wa Serikali wa kushirikiana na taasisi za fedha na wadau wengine kutekeleza sera na mikakati ya kuongeza tija katika sekta ya madini aliyosema imekuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.

“Mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa umepanda kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka wa fedha wa 2019/20 na inatarajiwa kufika zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2025. Serikali iko tayari kushirikia na taasisi za fedha kuongeza tija katika sekta ya madini,” alisema Gabriel

Aliwashauri wachimbaji wadogo nchini kuunganisha nguvu kimtaji kumudu siyo tu kufungua migodi ya kati na mikubwa, bali pia kutoa huduma katika migodi mikubwa ya Kimataifa kupitia sera ya local content inayoelekeza sehemu ya huduma migodini kutolewa na kampuni za wazawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles