BAMAKO, Mali
IDADI ya watu wanaokabiliwa na janga la njaa nchini Mali imeongezeka mara tatu, ukilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012, kwa mujibu wa ripoti ya taasisi 22 zinazojishughulisha na misaada ya kibinadamu.
Katika Mkutano wa Taasisi za Misaada ya Kibinadamu za kimataifa (Fongim), hali mbaya ya usalama, ukame, sambamba na athari za Corona vimesababisha njaa kwa watu milioni 1.2 kwa mwaka huu.
Familia nyingi zinashindwa kumudu vyakula kama mchele, ikielezwa kuwa bei yake imepanda kwa asilimia 22 katika baadhi ya maeneo.
Sehemu ya juhudi za Serikali ni katazo la wiki iliyopita, kwamba ni marufuku kusafirisha bidhaa za kilimo kwenda nje ya nje kipindi hiki cha balaa la njaa.