24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Al Ahly, Raja ‘kuuana’ Des. 22

CAIRO, Misri

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeitangaza rasmi Desemba 22, mwaka huu, kuwa ndiyo siku utakaochezwa mchezo wa Super Cup.

Mtanange huo utazikutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly, na Raja Casablanca ya Morocco ambayo ilitwaa taji la Kombe la Shirikisho.

Al Ahly waliitwaa ndoo ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga Kaizer Chiefs mabao 3-0 katika mchezo wa fainali, wakati vigogo wa soka la Morocco, Raja, walitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa kuitandika JS Kabylie mabao 2-1.

Hata hivyo, Al Ahly ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi ubingwa wa Super Cup ikiwa imelipeleka nchini Misri mara saba, ikiwamo mwaka jana kwa kuifunga RS Berkane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles